top of page

Msaada wa Dharura

Watoto huwa miongoni mwa makundi yaliyo hatarini zaidi katika kila hali ya dharura. Children for Life huhakikisha kuwa watoto walioathiriwa na migogoro ya kivita, mafuriko, njaa, mitetemeko ya ardhi, na milipuko ya magonjwa wanapatiwa huduma za dharura za kuokoa maisha ikiwemo matibabu, malazi, chakula na maji safi.

Ifuatayo ni orodha ya huduma na vifaa vinavyoweza kutolewa kulingana na aina ya mchango husika:

  1. Kibanda cha dharura, blanketi, mkeka wa kulalia, turubai na kamba — kwa Dola za Marekani 45 (US$45) kwa kila familia yenye watu 5.

  2. Vifaa vya usafi binafsi: sabuni ya mwili (Total Body Wash), povu la kunyoa (Shaving Lather), vitambaa vya kusafisha meno (Deep Cleaning Teeth Wipes), dawa ya kuondoa harufu ya mwili (Antiperspirant Deodorant), krimu ya kuzuia fangasi miguuni (Anti-fungal Foot Cream), vitambaa vya unyevu kuua bakteria (Anti-bacterial wipes), karatasi za chooni za usafi binafsi (Toilet Paper), mafuta ya kinga dhidi ya jua, vitambaa vidogo vya kufukuza wadudu, mafuta ya midomo yenye dawa na vidonge vya kutibu maji — kwa Dola za Marekani 20 (US$20) kwa kila mtu.

  3. Lishe maalumu ya siagi ya karanga kwa wiki tisa — kwa Dola za Marekani 5 (US$5) kwa kila mtoto.

  4. Kibanda cha mbao au turubai na viti, kwa watoto 30 — kwa Dola za Marekani 500 (US$500).

  5. Vifaa vya mtoto mchanga: sabuni ya mtoto, blanketi, kijitabu cha unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee, mavazi ya dharura, kofia na sweta — kwa Dola za Marekani 50 (US$50).

  6. Dawa za antibiotiki, chumvi ya kurejesha maji mwilini (ORS) na zinki — kwa Dola za Marekani 50 (US$50) kwa kila mtoto.

  7. Michezo kama mpira wa miguu au mpira wa kikapu na michezo mingine — kwa Dola za Marekani 40 (US$40) kwa kila mtoto au kundi la watoto.

  8. Vifaa vya shule: begi, kalamu, penseli, kifutio, daftari, kitabu, rula n.k. — kwa Dola za Marekani 60 (US$60) kwa kila mtoto.

  9. Matibabu ya minyoo na virutubishi vya madini — kwa Dola za Marekani 40 (US$40) kwa kila mtoto.

  10. Wolontia wanakaribishwa kutoa muda wao na nguvu zao katika kuwahudumia watoto kupitia Children for Life.

Kama sehemu ya mpango wa maandalizi ya dharura wa CFL, vifaa vilivyoorodheshwa hapo juu vinaweza kutolewa moja kwa moja au kupitia mchango wa kifedha.
Wito maalumu wa misaada ya dharura utatolewa kwa umma kupitia tovuti yetu na kwa wafadhili wa kudumu wa shirika.

Vifaa vya Makazi ya Dharura (Emergency Shelter Kits) vinajumuisha blanketi, mkeka wa kulalia, turubai na kamba kwa ajili ya kuwasaidia watu wasio na makazi katika nyakati za dharura.
Vifurushi vingine vinaweza kujumuisha sabuni, blanketi safi la mtoto, mwongozo wa unyonyeshaji, kofia iliyoshonwa kwa uzi, na ushauri kwa wazazi ili kuhakikisha watoto wachanga walioko katika mazingira ya dharura wanaendelea kuishi na kustawi.

Tupigie:​​

+255-763-205-703 or

+255-752-699-815

​Pata Ofisi Yetu: 

9 Dagoni Street, Mbweni JKT, Kinondoni District, Dar Es Salaam, Tanzania

Email: info@Childrenforlife.com

© 2015 na Children for Life 

© Copyright
bottom of page